ads

UTENZI: UTAMU WA KIVULI MWANDANI.



Ujumbe na kutumia,
Ujumbe huu pokea,
Ujumbe u maridhia,
Maneno yangu pokea.

Kwanza nina kusalimu,
Mwenzio ninayo hamu,
Haliyo kuifahamu,
Mpenzi wangu hamumu,

Na kwanza ni kuambie,
Mpenzi unisikie,
Hiyo hali yangu mie,
Kwanza nawe uijue.

Ninamaradhi moyoni,
Yanitesa akilini,
Tatizo mi sikuoni,
Hata kwa muda jamani.

Hali yangu sio njema,
Nionee na huruma,
Si bonde wala mlima,
Hali kwangu si nzima.

Lakini nikuambie,
Ya moyoni uyajue,
Sipendi uyachukie,
Mgongo ugeukie.

Majina yote maliza,
Ila hili laniliza,
Laazizi laaziza,
Hili linanimaliza.

Sifa zako kemkemu,
Kukimwa najidhulumu,
Namba moja ukarimu,
Uadilifu hamumu.

Dharau kwako pembeni,
Kila mtu mthamini,
Uzurio tabiani,
Wanichanganya jamani.

Karibu kwangu moyoni,
Karibu mpaka ndani,
Mpenzi mi taabani,
Hebu kwanza nithamini.

Hebu ingia furaha,
Furaha iso karaha,
Furaha pia na raha,
Mpenzi wangu karibu,

Najua upo hamuni,
Kulijua la moyoni,
Shaka iweke pembeni,
Sijakuweka rehani,

Mapenzi uvumilivu,
Yalojaa wingi wivu,
Napia usamehevu,
Uweke kando uvivu,

Lamoyoni nakujuza,
Na sipendi kukukwaza,
Nahofia litaoza,
Na moyo nitauliza.

Twasira naangazia,
La moyoni kukwambia,
Nakupenda maridhia,
Huna mfano dunia.

Sweety wangu maridhia,
Hali yangu waijua,
Upendo wangu pokea,
Mimi kwako nimetua.

Kila mti ndege wake,
Pia punguza makeke,
Napenda ufurahike,
Moyo wangu uridhike,

Ufungue moyo wako,
Hii sasa zamu yako,
Pokea mikono yako,
Nipende kipenzi chako

Sijapenda mali zako,
Wala si mavazi yako,
Moyo wangu upo kwako,
Nalipenda penzi lako.

Mangi yamejipitia,
Mengi nilikukosea,
Nisamehe maridhia,
Ubidamu wajua,

Samehe nilo kuuzi,
Nakupenda laazizi,
Kukuacha mi siwezi,
Kwako mimi ni mlinzi,

Moyo wangu taabani,
Jibulo nalitamani,
Maneno mengi kinywani,
Kuyasema yalo ndani.

Najua unipendavyo,
Wala sio kwenda ovyo,
Fikiri nikuwazavyo,
Ninakupenda ulivyo.

Nzuri taswira yako,
Nzuri taabia yako,
Heshimu wazazi wako,
Wakubwa jirai zako.

Uziri wako watosha,
Jicho langu kuliosha,
Pumzi pia kushusha,
Peke yako wanitosha.

Ila usinidhulumu,
Ukaja kunihukumu,
Penzi lako litadumu,
Sipendi unishutumu.

Maneo yangu sikia,
Furaha ukiridhia,
Nambie ukiiumia,
Mimi kwako naridhia,

Ukali maneno yangu,
Sikwako mpenzi wanu,
Mkarimu kwa wenzangu,
Na hiyo tabia yangu.

Tabibu maradhi yako,
Mahabuba mimi kwako,
Nieleze shida yako,
Mjuzi  wa afya yako.

Mengi nimejisemea,
Ila hapa nakomea,
Nikumbuke maridhia,
Moyoni hutaumia.

Mtunzi: MwinyiAbdallah
               (0655895599)
Email: mwinyiabdallah2012@gmail.com

Post a Comment

0 Comments