Nasema kwa tafsida, maneno napangilia
Kwenye moyo sina shida, nataka kuelezea
Mimi kwangu kawaida, ikiwa nimeridhia
Karibu ukaribie, chini moyo utulie
Karibu ukaribie, uliye mwema rafiki
Karibu ni hadithie, lipi lililokudhiki
Karibu name nijue, sihitaji halaiki
Kipenzi wewe ndo mie, moyo chini utulie
Kabla kuhadithia, niseme lilo moyoni
Huzuni imenitua, sijakuona machoni
Sina budi kuridhia, japo tiba siiyoni
Salamu ikikutua, kamwe usije nihini
Salamu zangu pokea, kutoka kwangu moyoni
Nafurahi kusikia, bado upo kivulini
Mwendo ukiufikia, mtangulize manani
Mola atakuridhia, ufurahi maishani
Ufupi maisha yetu, yata kinga rafiki
Rafiki alo mwenzetu, bila chembe unafiki
Ajue kilio chetu, machozi yakidiriki
Baraka za mola wetu, juu yetu zidiriki
Nakuomba samahani, nikate kwanza stori
Lipo jambo kiundani, kuwa nawe kama zari
Upendo uso kifani, kwa uzuri si hariri
Kwaheri naacha peni, nakupenda si utani.
Mtunzi: Mwinyi Abdallah Khatibu
0655895599
Email: Mwinyiabdallah2012@gmail.com




0 Comments