Maamkizi salamu, enyi vijana wenzangu
Salamu ilo na hamu, kwetu sisi islamu
Bila shaka mwafahamu, kuipokea salamu
Asalamu alaykumu, jamii waislamu
Siku sasa imefika, ndugu zangu tambueni
Swali mwinyi kalipika, majibu turudisheni
Name naanza hakika, majibu sikilizeni
Wanawake wetu sasa, wamekuwa mitihani
Ukimtaja huyo mussa, firauni pia jamani
Wanawake hiki kisa, ni mwalimu jamiini
Sasa pigeni msasa, jamii ihatarini
Wanawake wa zamani, ni kioo jamiini
Lakini sasa jamani, kioo cha wasanii
Wajiweka barazani, matangazo redioni
Waume hamuyaoni, nyinyi ndio marubani
Hebu kwanza anza kwako, mama na dada nyumbani
Wakumbushe na wenzako, ulo nao majirani
Kataza vikao kwako, vya umbea barazani
Mkeo na binti yako, na wajihifadhi ndani
Mtume muda mzuri, sokoni ende mchana
Usiku sio vizuri, kuna wengi wavulana
Vijana waso vizuri, wamejaa uvulana
Maneno yaso mazuri, wanapenda kutukana
Mpeleke na chuoni, elimu bora hakika
Ajue na quran, ni bora kuelimika
Weka darasa nyumbani, dini yao watashika
Nguzo tano zilo dini, swala bora wakishika
Pia na nyinyi vijana, vijana muso na ndoa
Tujitahidini sana, tukitaka kwenda oa
Dini ndio bora sana, uzuri utafwatia
Wanawake wengi sana, uzuri sio tabia
Waume nieleweni, na vichwa vitulizeni
Aisha huyu jamani, yu sawa na wazamani
Lakini huu mzani, sis indo tulawamani
Aisha huyu jamani, ni aisha wa zamani
Mwisho jibu limefika, jibu lisiloshakani
Hapa tunahitajika, waume kuwa mwanzoni
Wanawake bila shaka, ni kioo jamiini
Jibu limeshatoka, aisha yu wazamani
Mtunzi: Mwinyi abdallah
0655895599
Email: mwinyiabdallah2012@gmail.com
0 Comments