ads

SHAIRI: HERI YA KUZALIWA




1.
Mola namtanguliza, ujumbe kukupatia
Huenda ukakuliza, nakuomba vumilia
Mengine nakueleza, mengi umeyapitia
Chonde usijeibeza, muhimu kuzingatia
2.
Ninaweka kwanza pozi, moyoni nafikiria
Umeshazipanga ngazi, umepiga na hatua
Subira pia mapenzi, mola kakuongezea
Salamu hizi za enzi, moyo wako chini tua
3.
Mola amekuhifadhi, miaka imesogea
Kakukinga na maradhi, ukweli unaujua
Miaka leo yakidhi, hakika imetimia
Halijawa kwako udhi, penzi nilokupatia
4.
Miaka imetimia, muda mrefu wapita
Ngazi kuzipangilia, yakwanza hadi ya sita
Nakuomba vumilia, kusubiri sio vita
Hatua ilobakia, daima hauta juta
5.
Siku ulipozaliwa, hadi leo yatimia
Malezi uliyopewa, mzazi heko natoa
zuri umeumbiwa, mazuri umejazia
Mvua ulonyeshewa, dalili yake si jua
6
Nakshi naweka kati, nimefikia hatamu
Hii yangu ndo tamati, leo nimekusalimu
Nikiupata wakati, nitautunza kwa hamu
Umezaliwa Bahati, hongera sana hamumu

(MWINYI ABDALLAH)
Happy birthday to you, I wish u all the best my lovely honey

Post a Comment

0 Comments