ads

SHAIRI: MCHINJA NDIO RAISI


Usman Mchinja


Salamu zangu natuma, mjini na vijijini
Habari imeshavuma, wambali karibieni
Ugeni kwetu heshima, ni Baraka maishani
Ujumbe nitausoma, kura mchinja mpeni

Kwa mapana na marefu, ujumbe nitautoa
Huenda nikamsifu, pasipo kuweka doa
Huyu kijana nadhifu, walimu tunamjua
Nia yake takatifu, kura tukimpatia

Nia yake ni ya dhati, ubaguzi kuondoa
Ninaweka tashtiti, sera atawapatia
Ameweka mikakati, chuo mbele kusogea
Usiweke ati ati, kura yako kuitoa

Mchinja ni kiongozi, haki kuzipigania
Mchinja kwetu balozi, kura tukimpatia
Mchinja ndie mlezi, ukweli nawaambia
Mwalimu ndie mzazi, nani hilo asojua

Shime nyote wanachuo, mchinja kura mpeni
Tambua maendeleo, yataka mtu makini
Linalohitaji leo, kufika kesho ya nini
Kura ndio piganio, la haki yako chuoni

Kwa heshima taadhima, kura ninakuombeni
Wa cheti na diploma, mchinja kura mpeni
Shahada pia adhima, huyu kwenu si mgeni
Tumuombeni karima, awe raisi chuoni

Wapo wengi viongozi, walio mtangulia
Sipunguzi siongezi, mazuri walitugea
Pia nawapa pongezi, mema walotufanyia
Ninamuomba mwenyezi, Baraka kuwapatia

Tamati nimehatamu, rai yangu wanachuo
Tukihitaji matamu, hili ndo bora chaguo
Kura inakulazimu, mchinja uweke ndio
Mwinyi ndio mshairi, kura yako fanya siri.


Mtunzi: Mwinyi Abdallah
                0655 895599
Email: mwinyiabdallah2012@gmail.com

Post a Comment

0 Comments