ads

JUMANNE YA MCHINJA



Nguvu ya umma, nguvu ya wote

Amkeni amkeni, sauti ninaitoa
Naombeni nifateni, la mgambo limelia
Nataka nikwambieni, makosa kutorudia
Nitumie lugha gani, siku hii kuijua

Siku hii kuijua, kwanza ujue thamani
Haki zako kuzijua, mchinja mpe kidani
Jumanne utajua, thamani yake ni nini
Chelea mwana kulia, hulilia mitihani

Jumanne siku bora, kimbilia mjengoni
Jengo kubwa la duara, namba tatu mlangoni
Mchinja kampe kura, tupate mtu makini
Mchinja anayo dira, hima jama tuwahini

Jumanne ya thamani, nakuomba ushiriki
Mchinja tumuwekeni, tupate nguvu ya haki
Tusije sota jaani, kwa wanao pinga haki
Nguvu ya waote jamani, wengine watoke nduki

Uongozi wenye nguvu, huonekana mapema
Mwanamke ni shupavu, maamuzi kusimama
Mwanamke ni mwerevu, makamu wake ni mama
Maumbo yao angavu, wataweza kusimama

Huenda haujajua, jumanne kuna nini
Ndugu naomba tambua, hii siku ya thamani
Ndo siku ya kuingia, mkombozi wa chuoni
Mchinja unamjua, nguvu ya haki mpeni

Heshima ilo adhimu, ndugu nina kuombeni
Jumanne ni adhimu, mchinja mchagueni
Katuahidi matamu, kheri tukamuamini
Mchinja nguvu ya umma, mchinja raisi mwema

Mchinja raisi mwema, Tamati nimefikia
Mchinja raisi mwema, jumanne kuchagua
Mchinja raisi mwema, haki kuzipigania
Mwinyi kauli nasema, mchinja nguvu ya umma

Mtunzi: Mwinyi Abdallah
              0655895599
email: mwinyiabdallah2012@gmail.com 

Post a Comment

0 Comments