VITA VYA UHUD vita vya uhud vilikuwa ni vita vya pili baada ya vita vya Badr vilivyopiganwa mwaka 3 A.H, vilitokea karibu na mlima uhud na ndio maana vita hivi viliitwa kwa jina la ule mlima uhud. mtume (saw) katueleza haya kasema katika hadithi iliyopokelewa na Anas bin Maalik r.a na iliyotolewa na muslim, "hakika uhud ni jabali (mlima) unaotupenda na sisi tunaupenda" LENGO NA SABABU YAKE. Makafiri wa ki-Quraish walirejea kwao kutoka katika vita vya Badr na hali wamejeruhiwa na wamekasirika vibaya sana kwa kuuliwa wanaume wao, lakini kwa bahati yao nzuri umeokoka ule msafara wa mali yao. kwa hivyo wakakubaliana kwamba wachukue faida ya mali ya msafara ule uliokoka kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa kumpiga vita mtume SAW na maswahaba zake. na ili kukiondoa kizuizi cha biashara walichokifanya waislam katika njia ya madina mpaka sham. na mwenyezi mungu s.w.t ametukakikishia haya katika suratil Anfaal aya ya 36. "Hakika wale waliokufuru hutoa mali zao ili kuzuilia njia ya mwenyezi mungu. basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto na kisha watashindwa. na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam" MAKURAISHI WAANZA KUJIADAA NA VITA. fikra waliokuwa wakiifanyia kazi makuraishi tangu kumalizika kwa vita vya Badr ilikuwa ni kukusanya nguvu zake zote kwa lengo la kutekeleza pigo la kuvunjavunja litakalommalizia mbali Bwana mtume na maswahaba wake. kwa pigo hili takatifu watakuwa wameifangilia mbali na kuitokomeza kabisa dini yake hii mpya inayotishia utukufu na maslahi yao. wakaanza kufanya maandalizi ya motomoto kwa ajili ya kuitimiza fikra yao hii. wakaanza kuchanga pesa, kukusanya zana za vita na kuyapelekea wajumbe wake makabila ya waarabuyaliyo pembezoni mwao kuomba ushirikiano wao ili kuufanikisha makakati wao huu. miongoni mwa wajumbe (mabalozi) hawa alikuwa Abuu Azah; mshairi aliyetendewa wema na mtume kwa kumuuacha huru bila ya faida katika vita vya Badr. nae kwa kuonyesha shukrani zake kutokana na ukarimu aliotendewa akachukuaahadi ya kutokumsaidia yeyote dhidi ya mtume wala kuwa miongoni mwa adui zake. Akavunja ahadi aliyoweka mwenyewe akaenda pamoja na wajumbe wengine sehemu za kinaanah na tihaamah, kuwahamisha watu sehemu hizo kujiunga nao katika vita hii dhidi ya mtume. katika kipindi cha takribani mwaka mzima makuraysh waliendelea kukusanya mali, washirika na kutayarisha chakula kitakachokidhi mahitaji ya jeshi. mpaka vikafikia kiwango walichokusudia katika tathmini yao, wakaridhika na maandalizi hayo na kuona kuwa yamekamilika na kutimia. na kwamba yameweza kuwafikisha katika lengo lao na kuwahakikishia ushindi. karibu na kumaliza kwa mwaka wakatoka na jeshi linalotoa mvumo wa sauti ya kutisha kutokana na wingi wa idadi yake.walitoka pamoja na washirika wao wa tihaamah na kinaanah, pamoja na ndugu zao wa yaamini; wahabeshi wa Banil- mustwaliq na Bani-huun ibn khuzayma. wakaelekea madinah wakiwa na hamasa iendeshwayo na ukali wa ghadhabu ya kutoa pigo la kuvunjavunja na kuhilikisha. wanawake wa kikuraishi wao hawakubaki nyuma, walikuwa bega kwa bega na waume, baba na kaka zao wakiwahamasisha na kuwatia mori na ari. kiongozi wa wanawake hawa alikuwa ni HIndu bint utbah; mkewe Abuu sufiyaan ibn harb. miongoni mwa walioitika wito wa makurayshi dhidi ya bwana mtume na kujiunga na jeshi lao alikuwa ni Abuu Aamir Al Ausiy. huyu ni mtu wa kabila la Ausi ni katika makabila makuu ya waarabu wa madina, alikuwa mpinzani wa mtume na akikanusha utume wake. huko nyuma alijitia utawa akidai kumgonjea mtume aliyeletwa katika zama zao. Akiwatajia watu sifa za mtume ahuyo na akiwaambia: hakika zimekurubia zama za kuja kwake. bwana mtume (saw) alipohamia madina na sifa zake kuwadhihirikia maanswar kama walivyoambiwa wakamfuata na kumuamini. Abuu Aamir kuona hivyo, alimfania husuda mtume na kuukanusha utume wake. alikuwa ni kiongozi wa ausi kama alivyokuwa Abdallah ibn ubayyi kwa khazraj. wailin hawa wote walimfanyia hasadi mtume. lakini Abdullah ibn ubayyi aliingia katika uislam kinafiki na huyu alijitenga kabisa na uislam na kuendelea kuwa kafiri. akatoka na kundi lake la watu hamsini miongoni mwa vijana wa kiausi, akakaaa makka akiwaunga mkono nakurayshi na kuwahimiza kupigana na mtume. makurayshi walipoazimia kutoka kwenda uhud, Abuu Aamir aliwaahidi makurayshi kuwashawishi jamaa zake ausi kumtupa mkono bwana mtume saw. natoke katika safu ya waislam wajiunge na safu ya mushirikina yatakapokutana vitani makundi mwaili hayo. alitegemea kuyafikia haya kutokana na nafasi/cheo alichokuwa nacho huko nyuma kwa kabila lake. Akiamini kabisa kwa cheo chake hichoataweza kuigawa safu ya waislam. itaendelea sehemu ya pili............................................................................
0 Comments